July 15, 2025
Tangazo la Mafunzo kwa Ajili ya Usajili Kamili
MAFUNZO KWA AJILI YA KUWEZESHA WATHAMINI KUSAJILIWA KATIKA KUNDI LA USAJILI KAMILI NCHINI
Bodi ya Usajili wa Wathamini inapenda kuwatangazia Wathamini wote nchini kwamba inategemea kuendesha mafunzo kwa ajili ya kuwezesha Wathamini kusajiliwa katika kundi la Usajili Kamili, kama ilivyoainishwa katika Kifungu namba 28 (c) cha Sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini,Sura ya 318.