FRV HRV. Joseph Shewiyo
FRV HRV. Joseph Shewiyo

Wasifu

Kwa niaba ya Bodi, Menejimenti na Watumishi wa Bodi ninayo furaha kuwakaribisha kwenye tovuti yetu ambayo imeboreshwa kwa lengo la kuhabarisha umma kuhusu shughuli zinazofanywa na na Bodi ya Usajili wa Wathamini (VRB)

Bodi ya Usajili wa Wathamini (VRB) ni taasisi ya umma iliyoanzishwa kwa sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini Sura 138 kifungu cha 12 kwa ajili ya kusajili wathamini na kudhibiti kazi za uthamini nchini

Majukumu makuu ya Bodi ni kusajili wathamini katika ngazi mbalimbali baada ya kutathmini uwezo wao wa kielimu na uzoefu wa kazi, kuhamasisha maendeleo ya elimu ya uthamini na kusimamia/kutoa ushauri na kudhibiti utendaji kazi za uthamini na za wathamini nchini kwa lengo la kulinda maslahi ya wahusika wa uthamini Taifa, na umma kwa ujumla.

Ni imani yangu kuwa tovuti hii itasaidia sana kuonyesha kwa uwazi shughuli hizi zinazofanywa na Bodi hii kwa umma wa Watanzania ikiwa ni pamoja na kuongeza uelewa wa masuala yote yanayohusu Usajili wa Wathamini nchini Tanzania.

Tunashukuru kwa ushirikiano wenu na karibuni sana.

Joseph Shewiyo

Msajili wa Bodi.