Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi afungua Rasmi Mkutano Mkuu wa Sita wa Wathamini nchini
Mhe. Kaspar Mmuya Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (MB.) amefungua Mkutano huo wa Sita wa Wathamini wenye mada kuu "Taaluma ya Uthamini katika Nyakati za Mabadiliko ya Kiteknolojia" ambapo amewapongeza wajumbe na menejimenti ya Bodi kwa kazi nzuri na kubwa wanayoifanya katika Bodi ya Wathamini na amewataka Wathamini nchini kuacha kufanya kazi kwa maslahi yao binaafsi bali wafanye kazi za Uthamini kwa weledi na kuzingatia maadili ya fani ya Uthamini ili kuleta matokeo chanya kwa Watanzania kwa ujumla na kuzingatia mifumo ya kidigitali. Mkutano huo wa siku mbili umefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Morena Hoteli mkoani Morogoro kuanzaia tarehe 04 - 05 Desemba, 2025.