WATUMISHI WA BODI YA USAJILI WA WATHAMINI WASHIRIKI UPANDAJI WA MITI

Imewekwa: 02 February, 2026
WATUMISHI WA BODI YA USAJILI WA WATHAMINI WASHIRIKI UPANDAJI WA MITI

Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wathamini HRV. Joseph Shewiyo leo januari 27, 2026 amewaongoza watumishi wa Bodi katika zoezi la upandaji lililoongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo na Naibu wake Mhe. Kaspar Mmuya..

Zoezi hilo lenye kauli mbiu "Kesho yetu inaanza na mti unapopanda leo, panda mti kwa Maendeleo Endelevu ya Makazi". Ambapo Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo amesema, Wizara yake inashiriki zoezi la upandaji miti kuunga mkono juhudi za Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  mwanamazingirz namba moja kutunza mazingira hasa ikizingatiwa kuwa leo januari 27,2026 ni siku yake ya kuzaliwa.

Settings