BODI YA USAJILI WATHAMINI YAFANYA KIKAO CHA 23 CHA BODI

Imewekwa: 21 November, 2025
BODI YA USAJILI WATHAMINI YAFANYA KIKAO CHA 23 CHA BODI

Leo tarehe 21 Novemba, 2025, Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wathamini (VRB) FRV. Zidikheri Mndeme ameendesha kikao,kilichofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi uliopo Mtumba jijini Dodoma. Kikao hicho kimehudhuriwa na Msajili wa Bodi, Wajumbe wa Bodi na Menejimenti ya Bodi.

Katika kikao hicho, Bodi imejadili mambo mbalimbali ya kitaaluma na maadili ya Uthamini pamoja na kupitisha Wathamini wapya katika ngazi ya Wathamini wa Awali(PRV), Makampuni ya Uthamini na Fundi Sanifu (TV).

Settings