UZINDUZI WA AWAMU YA TATU YA BODI YA USAJILI WA WATHAMINI
Bodi ya Usajili wa Wathamini imefanyikiwa kuzindua awamu mpya ya Wajumbe wa Bodi ambao wameapishwa na Mhe. Jerry W. Silaa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, ambap wajumbe hao watashirikiana na ofisi ya Msajili wa Bodi katika kutekeleza majukumu mbalimbali ya Bodi. Katika tukio hilo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry W. Silaa amewapongeza wajumbe wapya waliochaguliwa na amewahasa wafanye kazi kwa Uweledi na ustadi wa hali ya juu ili kuisaidia Bodi iweze kufikia malengo yake na kuikuza sekta ya Uthamini nchini Tanzania. Bodi mpya sasa itaongozwa na FRV. Zidikheri M. Mndeme Mwenyekiti wa Bodi na FRV. Dkt. Upendo Matotola atakuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi.
Aidha, tukio hilo limeambatana na tukio la kuwaaga wajumbe waliomaliza muda wao wa majukumu ya kiutendaji ambapo Mhe. Jerry W. Silaa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amewapongeza na kuwashukuru wajumbe hao kwa kujituma na kujitoa kwao kwa dhati kwa kufanya shughuli za Bodi kwa kipindi cha muda wao wa uongozi pia amewaomba isiwe mwisho wa kujitoa na kushirikiana na Wajumbe wapya katika shughuli na mawazo chanya ya kuijenga Bodi na taaluma ya Uthamini nchini. Tukio hili limefanyika tarehe 07 Juni, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete Convention Center, jijini Dodoma.
Tukio hilo limehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Antony Sanga pamoja viongozi mbalimbali wa kidini na sekta ya Ardhi, Watumishi wa Wizara ya Ardhi, watumishi wa Bodi ya Usajili wa Wathamini, wawakilishi katika sekta ya Uthamini pamoja na Waandishi wa habari.