emblem

The United Republic of Tanzania

VALUERS REGISTRATION BOARD

HAFLA YA KWANZA YA WATHAMINI WA KUDUMU (FRV’S)


Bodi ya Usajili wa Wathamini iliandaa Hafla ya kuwatunuku vyeti Wathamini wa Kudumu waliofuzu mafunzo na kutimiza vigezo vyote vya Bodi kwa ajili ya kupata Usajili wa Kudumu .

Hafla hiyo ilifanyika Aprili 6, /2022 katika ukumbi wa Royal village Dodoma - Tanzania ambapo Mgeni rasmi alikuwa Mhe. David Ernest Silinde Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

Aidha mahafali hiyo ilihudhuriwa na Bi. Evelyne B. Mugasha Mthamini Mkuu wa Serikali, Dr. Cletus Eligius Ndjovu Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Wathamini, Wajumbe wa Bodi, Bw. Joseph I. Shewiyo Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wathamini, walimu wa wahitimu pamoja na wadau mbalimbali wa Uthamini nchini.