emblem

The United Republic of Tanzania

VALUERS REGISTRATION BOARD

FOURTH ANNUAL GENERAL MEETING OF VALUERS REGISTRATION BOARD


Bodi ya Usajili wa Wathamini (VRB), imefanya Mkutano Mkuu wa Nne wa Mwaka ambapo Mgeni Rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassimu Majaliwa (MB), amewataka Wathamini wote nchini wawe waadilifu , wenye uweledi na wazingatie miiko ya taaluma katika kazi zao za kila siku na kwamba kazi ya Uthamini si ya wababaishaji au vishoka, hivyo basi kila Mthamini hana budi kuthamini na kuheshimu taaluma yake.

Pia, Mhe. Kassimu Majaliw a amesema kuwa Wathamini ni watu muhimu katika kufanyikisha mipango ya maendeleo ya Taifa. Amesema hayo alipokuwa akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa Nne wa Wathamini wenye siku mbili (09 - 10/11/2023) uliobeba Dhima ya "Utafiti na Uchimbaji Madini kwa Maendeleo Endelevu ya Taifa: Tathmini ya athari za Haki - ardhi, Thamani na Fidia ya Ardhi". uliofanyika alhamisi tarehe 09 Novemba, 2023 katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.