emblem

The United Republic of Tanzania

VALUERS REGISTRATION BOARD

Mthamini kama shahidi wa kitaalam


Bodi imeandaa mafunzo kuhusu Mthamini kama mtaalam mshahidi wa Mahakamani ambayo yamefanyika katika Hoteli ya Morena Morogoro tarehe 23 na 24 Februari, 2023. Mafunzo haya yamehusisha Wathamini wote na wadau wengine wa ardhi na uendelezaji milki nchini. Dhima ya mafunzo haya ni “Mthamini kama shahidi wa kitaalam” (Valuer as an expert witness). Washiriki wa mafunzo haya walipatiwa alama mbili (2) za mafunzo.

Mafunzo haya yalihudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi FRV. Dkt. Cletus Ndjovu, yamelenga kumsaidia mthamini kama mtaalam kuweza kusimama mahakamani na kutoa ushahidi katika shughuli zake pale inapohitajika kufanya hivyo pia kupitia mafunzo haya wathamini wamepata muda wa kuchangia mawazo, ushauri na maoni juu ya uendeshaji wa mafunzo ya Bodi pamoja na shughuli za Bodi ili kuongeza ufanisi wa shughuli mbalimbali za Bodi. Aidha, Bodi inaendelea na mchakato wa kutoa mafunzo kwa wathamini wa ngazi zote waliosajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wathamini ili kusaidia kuongeza ufanisi na ukuaji wa sekta ya Uthamini nchini ambapo mafunzo mengine yanatarajiwa kutolewa ifikapo mwezi mei 2023.