• Mafunzo ya Kitaaluma kwa Usajili

Bodi imeandaa mitaala na taratibu za mafunzo zinazotakiwa katika kufanya mitihani ya kitaaluma. Aidha, Bodi inashirikiana na vyuo vinavyotoa mafunzo ya taaluma za kithamini au wakufunzi na wataalamu wengine katika kuhakikisha kuwa elimu bora inatolewa.

  • Mitihani ya Kitaaluma kwa Usajili

Kufuatana na Taratibu na Sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini ya Sura 138, usajili wa wana taaluma wa uthamini hufanyika baada ya kufanya mitihani ya Bodi katika ngazi mbalimbali.