Katika kutoa mafunzo endelevu kwa wathamini, Bodi inafanya yafuatayo:

  • Inawasiliana na taasisi zinazotoa mafunzo ya uthamini na kujadiliana namna bora ya kuboresha taaluma ya uthamini hapa nchini na kuhusisha taasisi za nje ya nchi pia,
  • Inapanga na kuendesha kozi, mikutano, semina, makongamano ambapo masuala mbalimbali ya kitaaluma yanajadiliwa; na
  • Inaandaa machapisho na kusambaza nyaraka za kazi za uthamini kwa wathamini na umma kwa ujumla.