emblem

The United Republic of Tanzania

VALUERS REGISTRATION BOARD

BUSINESS VALUATION AND PROFESSIONAL ETHICS


Bodi ya Usajili wa Wathamini (VRB) imeendesha mafunzo endelevu ya Uthamini wa biashara na maadili ya kitaaluma "Business Valuation and Professional Ethics" tarehe 15 -16/06/2023.

Bodi ya Usajili wa Wathamini (VRB) imeendesha mafunzo endelevu ya Uthamini wa biashara na maadili ya kitaaluma "Business Valuation and Professional Ethics" ikishirikiana na wakufunzi mahiri katika sekta ya Uthamini nchini, wakufunzi hao ni FRV. Dkt. Hidaya Kayuza, FRV. Sultan Mndeme, FRV. Dkt. Vianey Mushi, FRV. Robert Mwakasisya na wakili msomi Adv. Tarsila Asenga. Mafunzo yaliyunguliwa na kufungwa na mwenyekiti wa Bodi FRV. Dkt. Cletus Ndjovu.

Mafunzo hayo yameendeshwa kwa siku mbili tarehe 15 - 16/06/2023 katika ukumbi wa Mount Usamabara hotel jijini Tanga na kuhudhuriwa na zaidi ya Wathamini 120. Kuhudhuria mafunzo yanayotolewa na Bodi ni muhimu kwa kila mthamini aliyesajiliwa na Bodi ili kila mthamini aweze kukuza taaluma yake na taaluma ya Uthamini nchini pamoja na kujenga mahusiano chanya baina ya wathamini na makampuni ya Uthamini nchini.